Maelfu wapinga kombe la dunia Brazil
Polisi watibua
maandamano Brazil
Polisi wa kupambana na
ghasia wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanaji
katika barabara za miji ya Sao Paolo na Rio de Janeiro walipinga mfumuko wa
gharama ya uenyeji wa kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini Brazil.
Baadhi ya waandamanji
walipura mawe na kuchoma magurudumu ya magari na kufunga mabarabara ya miji
wakidai serikali haikuzingatia matakwa ya wananchi kama vile elimu sekta ya
afya na muundo msingi.
Katika tukio
linaloibua hofu ya kuwepo kwa usalama wafanyikazi wa umma na walimu walijiunga
na waandamanaji katika miji yote mikuu ikiwemo mji mkuu wa Brasil.
Wengi wao waliahidi
kurejea mabarabarani kadri mchuano huo unavyosongea .
Mwaka uliopita
takriban watu milioni moja walishiriki maandamano wakilalamikia ufisadi
ubadhirifu wa mali ya umma na ongezeko la gharama ya uandalizi wa kipute hicho
cha fainali ya dimba la dunia .
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 12 June.
Waandamanaji walianzia
Sao Paulo,karibu na uwanja wa Corinthians Itaquera karibu na mtaa wa Itaquera .
Uwanja huo wa
Corithians ndio utakaoandaa mechi ya ufunguzi wa kombe la dunia mwaka huu
tarehe 12 juni.
Polisi watibua
maandamano Brazil
Kwa mujibu wa shirika
moja la kijamii linaloandaa maandamano hayo Homeless Workers Movement
waandamanji wanaitaka serikali kutumia fedha katika ujenzi wa nyumba .
Kulingana naye
hangependa viwanja vilivyogharimu mabilioni ya dola viharibiwe ila wafanyikazi
wanaojenga viwanja hivyo wajengewe nyumba kuambatana na ubora wa shirikisho la
soka duniani FIFA.
Serikali imepinga
uhisano wowote kati ya maandamano haya na kombe la dunia .
Waziri wa michezo Aldo
rebelo amenukuliwa akisema kuwa ameona matakwa ya waandamanaji na ikampa
matumaini maandamano hayo hayataathiri ujio wa takriban watalii milioni tatu na
wageni laki sita wanaotarajiwa kuzuru miji itakayoandaa mechi za kombe la
dunia.
Hata hivyo maandamano
haya yanawadia wakati ambapo serikali inakabiliwa na mgomo wa wafanyikazi wa
umma na hata polisi katika jimbo la Pernambuco