MATUKIO YA KUSIKITISHA NDANI YA WILAYA YETU, KIKUBWA MUNGU TUNUSURU NA MAMBO HAYA YASIENDELEE.

Mwezi wa tano (Mei) 2014 matukio ya kusikitisha yamejitokeza ndani ya wilaya yetu ambapo
  • ·         Mke alimuua dada wa mume wake yaani wifi ake katika kijiji cha Ruganzo,
  • ·         Mfanyabiashara  anayejulikana kwa jina la Mawazo alijinyonga maeneo ya Ngara mjini.
  • ·         Mtu mmoja alikunywa sumu huko maeneo ya Mkanywampezi(Mrugwanza)
  • ·         Anayeuguza kufa gafla na kumuacha mgonjwa hai Mrugwanza
  • ·         Pia mfanyakazi wa ndani (house girl) amekabidhi mtoto kwa bosi wake na kwenda kujinyonga  maeneo ya Girrafe bar Ngara


Hayo matukio yote yametokea ndani ya mwezi huu wa tano, na hatujui utaishaje, jamani tuiombee Ngara yetu inakoelekea siko.
 
Top