CHUO
KIKUU CHA MWENGE CHATWAA KOMBE LA MFUKO PENSHENI WA PSPF MKOANI KILIMANJARO.
Timu
ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Mwenge kimetwaa ubingwa huo katika mchezo
uliwakutanisha na timu ya mpira wa miguu ya chuo cha ushirika na
biashara(MUCCOBs) ambapo timu ya Mwenge imeshinda kwa ushindi wa gori mbili kwa
bila( mbili sifuri) na kutwaa kombe hilo katika mchezo ulochezwa leo saa kumi jioni
katika uwanja wa ushirika mjini Moshi
PSPF
imeahidi kuendeleza mashindano hayo yaliyoanza mwaka huu hivyo timu za vyuo
vikuu mkoani Kilimanjaro zijiandae kushiriki katika michuano itakayofata.
Pia
katika burudani hiyo timu nyingine za mpira wa wavu na mpira wa pete
zimechuana, ambapo timu ya mpira wa wavu ya chuo cha ushirika, imeshinda kwa
seti tatu kwa moja dhidi ya timu ya Mwenge ya mpira wa wavu. Pia timu ya mpira
wa pete ya chuo cha Mwenge imeshinda kwa jumla ya magori 40 kwa 20 dhidi ya
timu ya chuo cha ushirika.
Hongera
sana chuo kikuu cha Mwenge.