Serikali ya Tanzania imethibitisha
mradi wa Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni.
Umekua ni usafiri mwingine mzuri na wenye starehe yake kama
ukipata nafasi ya kuutumia kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza
Dubai na kwengineko ambako kuna watu wengine wanategemea sana kuutumia na
kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza shughuli zao
manake hamna foleni.
Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa
Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi
BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na
namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake
wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi,
barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni
kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu
na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake?
manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar
na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme
ni lazima uwepo kwa saa 24′
Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe
Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa
tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza
na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu
moja.
Source: Millad Ayo
website