Wiki kadhaa baada ya kumtimua
kocha David Moyes klabu ya Manchester united wanakaribia kumtangaza kocha wa
timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal kuwa meneja mpya wa timu hiyo.
Mholanzi
huyo tayari ameshakubali kuchukua madaraka ya ukocha Old Trafford lakini bado
ana kazi ya kuiongoza Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia na maandalizi
ya kujiandaa na michuano hiyo yamesababisha dili lake na United kuchelewa
kukamilika.
Mwanzoni
iliripotiwa kwamba angetambulishwa mwishoni mwa wiki hii lakini badala yake
ameendelea kubaki nchini Uholanzi na inaaminika sasa atatambulishwa wiki ijayo
baada ya mchezo wa kirafiki.
Jana
Ryan Giggs ambae ameshika madaraka ya ukocha kwa muda alisafiri mpaka Uholanzi
ambapo alikutana na Van Gaal mjini Noordwijk kwa ajili ya kuzungumza juu ya
Giggs kupewa madaraka ya kocha msaidizi pamoja na mipango ya usajili msimu ujao.