Maandamano ya wananchi wa mji mdogo wa sirari wilaya ya Tarime mkoani Mara waliotaka kujua chanzo cha mauaji ya kijana mmoja mkazi wa eneo hilo ambaye anadaiwa kukamatwa na Jeshi la polisi na kisha mwili wake kukutwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime yamesababisha vurugu kubwa na kusimama kwa shughuli mbalimbali za kijamii kwa saa kadhaa
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la kitandika Ryoba anadaiwa kukamatwa siku nne zilizopita na askari wa jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa tuhuma za kukutwa akicheza kamali lakini tangu siku ya tukio hilo kijana huyo hakupatikana hadi taarifa za kifo zilipowafikia ndugu zake na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha Maiti katika hospital ya wilaya ya Tarime
Taarifa hizo zilisababisha wananchi wa eneo hilo kufanya Maandamano ikiwa ni njia ya kushinikiza jeshi la Polisi kueleza chanzo cha kifo cha kijana huyo ambapo jeshi la polisi liliingia kati kuzima maandamnao hayo hali ambayo ilisababisha wananchi hao kuifunga barabara kuu ya inayotumika kwa safari za Mwanza,Tarime na nchi jirani ya Kenya kwa kutumia Mawe lakini pia wakichoma matairi ya Magari.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Tarime Rorya Kamishana msaidizi Mwandamizi Justus Kamgisha amesema Mtuhumiwa huyo kitandika Ryoba baada ya kukamatwa alifikisha kituo cha Polisi kuhojiwa na wakati Mahojiano yakiendelea alidai kujisikia vibaya ambapo nalikimbizwa hospital na wakati anapatiwa matibau akafariki dunia. -
Credits:mwanawaafrika blog