Wastani wa takribani wanawake mia moja mkoani Singida hufanyiwa vitendo vya ukatili na wanaume zao ikiwemo vipigo ikifuatiwa na ubakaji, na utupati watoto wa changa kwa wazazi kwa madai ya kutelekezwa na wenzi wao.
Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi dawati la jinsia mkoani Singida Asp Ireen Mbwatilo katika ripoti ya utekelezaji wa majukumu yake na changamoto za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na mpango wa ushirikiano baina ya dawati na asasi wadau wa masuala ya kijamii na maendeleo yake kwa kupunguza watoto wa mitaani, uzazi wa mpango na uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Aidha katika ufafanuzi wa matukio umetajwa umaskini, elimu duni na mfumo dume miongoni mwa wamaume mkoani humo kuwa vichocheo vya kushindwa kuwajibika kwa familia zao na kuzalisha watoto wengi wa mitaani kwa kushindwa kuwaendeleza.
Hata hivyo katika vijiji mbalimbali baadhi ya wanaume walikiri awali kuwa vinara wa vipigo kwa wenzi wao huku wakieleza kuelimika kupitia mradi wa ushiriki wa wanaume kwa afya ya uzazi na ujinsia TIMEP unaotekelezwa na serikali ya Sweden kupita asasi za kiraia na kuahidi kuwa mabalozi wa vita ya ukatiri wa kijinsia kwa jamii yao.