MWANAFUNZI aliyefahamika kwa jina la Athony John (14) mkazi wa kijiji cha Ihalo kata ya Ilola tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga Mkoani hapa aliyekuwa akisoma Darasa la tano katika Shule ya Msingi Ihalo amefariki Dunia wakati akiogelea kwenye bwawa la Maji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Agost 10 mwaka huu majira ya Saa tisa Jioni wakati mwanafunzi huyo akiogelea kwenye bwawa la maji kuzama na kisha kusababisha kifo chake.

Kamugisha alisema kijana huyo akiwa peke yake alikuwa anaogelea katika bwala la maji lenye kina kirefu ambapo alishindwa kuongelea na kuanza kunywa maji hayo na kisha kuzama hadi kupelekea kifo chake.
 
Top