Kumekuchaaaa ndani ya Ngaraaaaa! ule mdahalo wa kihistoria unaoandaliwa na Chuo cha Madini Sekhasa kwa ushirikiano na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu umewadiaaaaaaa! ni ndani ya ukumbi wa City Life tar 15/08/2014 ambapo mada "Tatizo la ukosefu wa ajira na umasikin unaowakumba vijana hususani wa wilaya ya Ngara, kipi kifanyike kunusuru?
watoa mada ni Dr. Philemon Sengati (muhadhili chuo kikuu cha Dodoma(UDOM), Dr. Peter Bujari kutoka Human Development Trust, Dr. Gresmus Sebuyoya, viongozi wa halmashaur ya wilaya ya ngara (mkurugenz, afisa mipango nk, Sabrah Khalfan mmiliki wa Sekhasa mining, Helena Adrian(mmilik wa Lake High school), mr. Alex Gashaza (mkurugenz Gashaza Construction Company, Kabanga Nickel Company, na wengine wengiiii, hakuna kiingiliooo,,,,, ni bureeee kabisaaaa.
Aidha mdahalo huo sio wa kisiasa na hoja zote za kisiasa hazitakubaliwa. Hili kama wasomi na waandaaji wa mdahalo tumelijua mapema na pia siasa imechangia mambo mengi ya maendeleo kukwama. wananchi wote wa wilaya ya Ngara na wengine kutoka nje mnaarikwa kuhudhuria mdahalo huo pia hi ni njia ya ukombozi wa vijana wasomi kwa wilaya yao kwa kuchangia elimu waliyoipata kwa maendeleo.
Elimu ya ujasiriamali itatolewa siku hiyo maana kuna wataalamu mbalimbali wamebobea kwenye nyanja hizo za uchumi na maendeleo kutoka vyuo na sehemu mbalimbali.
Wafanyakaz wa umma, vijana wajasiriamali, wakulima na wengine wote mnakaribishwa mawazo yenu ni muhimu sana katika mdahalo huo.