Hali ni tete sana eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Katavi kugongana uso kwa uso. Dreva wote wa mabasi hayo wamefariki hapo hapo, mmoja akiwa amekatika kichwa.
Abiria kadhaa wakiwa wamenasa katika mabasi hayo, baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu. Abiria wapatao watano wamefariki hapo, na majeruhi zaidi ya 30 wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
Updatehadi sasa mganga mkuu wa hospital ya mkoa wa tabora amedhibitisha kuwa waliofariki ni watu 16 tu, na majeruhi 70.