Bomoabomoa Kawe, wananchi walia na kiwango cha nauli wanachopewa
Wakazi wa eneo la Kawe Mzimuni waliokuwa wakiishi kwenye nyumba za Tanganyika Packers jana wameondolewa kwenye nyumba hizo ili kumpisha mmiliki wa eneo hilo ambaye ni shirika la Nyumba la Taifa- NHC.
NHC imetoa kiasi cha shilingi laki moja kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo ili wajisitiri lakini wakazi hao waliopokea kiasi hicho cha fedha wamesema hakitoshelezi mahitaji yao ya kuanza maisha mapya kwenye maeneo mengine
Azimio Milinga ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mzimuni ambaye pia ni miongoni mwa wananchi waliokumbwa na mkasa huo hii leo
Hata hivyo wananchi wengine wa eneo hilo wamesema pamoja na kwamba walikuwa na taarifa ya kuhamishwa kwenye eneo hilo, kitendo kilichofanyika jana cha wao kutakiwa kuhama kwenye makazi yao ni cha ghafla.