Ni muonekano wa msuluru wa Malori katika Mpaka wa Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera unaounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda ambapo Upimwaji na Ukaguzi kuhusu Ugonjwa wa Ebola umekua ukifanyika.

Habari za kuzuka kwa ugonjwa hatari wa ebola katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ni za kutia hofu na kwa Tanzania bado mikakati dhabiti haijatekelezwa kwani licha ya Idara za Afya kutoa maelezo ya nini Kifanyike mtu atakapogundulika na Ebola ,lakini maeneo ya Mipakani bado Ukaguzi wake haujaimarishwa ikilinganishwa na Nchi ya Rwanda unavyofanyika.


Serikali ya DRC imesema watu wawili walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo kaskazini mwa nchi hiyo wamefariki dunia, huku kukianza kujitokeza wasiwasi mkubwa kwa nchi zilizoko katika eneo la Afrika Mashariki kuhusu uwezekano wa kukumbwa na ugonjwa huo ambao mpaka sasa hauna chanjo wala tiba.


SASA Katika kukabiliana na habari ambazo bila shaka zimepokewa kwa mfadhaiko mkubwa na serikali zote zilizo katika ukanda huo kutokana na ukweli kuwa, hadi kufikia wikii ugonjwa huo wa ebola uliozuka mwezi uliopita ulikuwa umeua watu 1,427 katika nchi za Guinea, Sierra Leone, Liberia na Nigeria.









 
Top