Zaidi ya wanyama 360 wamekufa kutokana na kugongwa na magari katika hifadhi ya taifa ya Mikumi kwa kipindi cha mwaka mmoja licha ya serikali kuweka matuta na vibao vya kudhibiti mwendo kasi katika barabara kuu ya Morogoro iringa inayopita katikati hifadhi na kusababisha idadi ya wanyama kuendelea kupungua katika hifadhi.
Muikolojia mkuu wa hifadhi ya wanyama Mikumi Crypin Mwinuka amesema takwimu zinaonyesha kila siku mnyama mmoja anakufa kwa kugongwa na magari ingawa wameweka alama za tahadhari zikiwataka madereva kupunguza mwendo kasi lakini bado baadhi ya madereva wanakaidi tahadhari hizo na kugonga wanyama wakiwemo Simba na Chui na kusabisha idadi yao kupungua katika hifadhi.

Nao madreva wanaotumia barabara ya Morogoro Iringa kupitia katikakati ya hifadhi hiyo ya mikumi wamesema matuta tuu hayatoshi wameshauri Tanapa kuweka vifaa maalumu vya kubaini madereva wanaogonga wanyama ili wachukuliwe sheria ikiwemo kulipa faini ili kupunguza matukio ya wanyama kufa kwa ajali za barabarani.
 
Top