Pichani ni akina mama kutoka katika manispaa ya Shinyanga wakiwa wamebeba ndoo za maji kichwani kabla ya kuanza mashindano ya mbio za baiskeli huku wamebeba ndoo za maji kichwani kuzunguka uwanja wa ccm kambarage Mjini Shinyanga siku ya Sikukuu ya wakulima Nane Nane katika mkoa wa Shinyanga.Mashindano hayo ya mbio za baiskeli yalikuwa yamedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI AKINA MAMA WAKIENDESHA BAISKELI HUKU WAMEBEBA NDOO ZA MAJI KICHWANI KUZUNGUKA UWANJA WA KAMBARAGE


Katika mbio hizo za kuendesha baiskeli huku umebeba ndoo ya maji kichwani mshindi wa kwanza alikuwa Makirikiri Joseph(wa kwanza kulia) ambaye amejinyakulia shilingi laki moja na nusu,mshindi wa pili Christina Giti (katikati)ambaye amepata shilingi laki 1,mshindi wa tatu Joyce Bundala( wa kwanza kushoto) aliyejinyakulia shilingi elfu 80


Mbali na kuandaa mshindano ya mbio za baiskeli kwa akina mama wakiwa wamebeba ndoo kichwani,TBL pia waliandaa mbio za baiskeli kwa watu wenye ulemavu.Pichani washiriki wa mashindano hayo wakijiandaa kuanza mpambano wakizunguka uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga


Kulia ni mshindi wa Kwanza Makende Derema aliyejinyakulia shilingi laki 1 na nusu,mshindi wa pili Ngalu Ngamba(katikati) aliyondoka na shilingi laki 1,mshindi wa tatu Peter Thomas( wa kwanza kushoto) aliyejinyakulia shilingi elfu 80




Katika kusherehekea sikukuu ya nane nane mkoani Shinyanga TBL pia waliandaa mbio za baiskeli kwa wanamme za umbali wa kilomita 220.Pichani washiriki wakijiandaa kuanza safari kutoka Uwanja wa ccm Kambarage Shinyanga mjini kwenda Kahama kisha kurudi mjini Shinyanga ,ambapo unaambiwa walitumia masaa 6 na dakika 6 tu
 
Top