MATUKIO:-MTOTO HUYU KAIBIWA ,LEO SIKU YA 10,HAJULIKANI ALIPO
Mtoto Emmanuel Jeremiah, miezi 9 mkazi wa kata ya Rwamgasa - Mkoani Geita ambaye hadi sasa hajulikani alipo
Mtoto Emmanuel Jeremiah, miezi 9 mkazi wa kata ya Rwamgasa - Mkoani Geita
Helena Asunga mkazi wa Mgusu - Geita anayedaiwa kumuiba mtoto Emmanuel
IKIWA ni siku chache tu baada ya malunde1 blog kuripoti kushamiri kwa vitendo vya kuibiwa kwa watoto wadogo katika Mkoa wa Geita na kupelekwa kusikojulikana tukio jingine limetokea tarehe saba mwezi huu majira ya saa nane mchana ambapo mtoto Emmanuael Jeremiah miezi (9) mkazi wa Mgusu kuibiwa na kutokomezwa kusiko julikana mpaka sasa.
Akizungumzia juu ya tukio hilo juzi baba mzazi wa mtoto huyo Jeremia Emmanuel alisema siku hiyo jirani yake aliyejulikana kwa jina la Helena, Asunga miaka(32) mjaluo alimkuta akiwa nje ya Nyumba yao na kumchukua mtoto na kutokomea naye kusiko julikana mpaka sasa.
Jeremia aliongeza kuwa yeye na mke wake Lilian Jeremia walikuwa ndani ya nyumba na walipotoka nje walikuta mtoto wao hayupo na kuambiwa na jirani yake kwamba kachukuliwa na Helena na hawakuanza kumtafuta kwani ilikuwa ni kawaida jirani huyo huwa anamchukua na kumrudisha.
Alisema ilipofika saa kumi jioni siku hiyo alikwenda kwa jirani huyo na kuuliza kama Helena yupo na kukuta hayupo na alipouliza mtoto wake aliambiwa hajafikishwa pale na kuanza kumsaka kila kona lakini jitihada za kumpata ziligonga mwamba na kwenda kuripoti katika kituo cha polisi Mgusu na kupewa RB BKR/IR/68/2014.
Matukio ya kuiba watoto katika mkoa wa Geita yanazidi kushamiri huku wanaoiba huwapoteza watoto hao na kuwataka wazazi wao kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili warudishe au huwaelekeza walipo mara baada ya kutoa.
Jeshi la polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kuibiwa kwa mtoto huyo unaendelea na mtuhumiwa bado anatafutwa.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita