Aidha ulianzishwa utaratibu wa kutumia teknolojia ya university management system(ums) kusajiri taarifa za wanachuo na pia kutumia njia hiyo kutuma matokeo ya wanachuo hao. Na utaratibu huo ulimlazimu kila mwanachuo kulipia kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwaka wa masomo ili apate huduma hizo ikiwemo na huduma ya wireless chuoni hapo. Kinachosikitisha ni pale ambapo tangu wanafunzi hao wapo mwaka wa pili huduma hiyo ya matokeo imekuwa na matatizo ambapo asilimia kubwa walitegemea matokeo yabandikwe kwenye mbao za matangazo.
Ila kwa sasa kilio kimekuwa kikubwa maana wanafunzi hao wamehitimu na tegemeo lao kubwa ilikuwa wapate matokeo ya mwisho kupitia ums lakini cha kusikitisha baadhi wamewekewa matokeo nusu yaani course chache na kuacha nyingine kusikojurikana, wakati wengine wamewekewa matokeo ya watu wengine, na wengine wamewekewa matokeo ya semester (muhula wa kwanza) yamejirudia mara mbili na kilichotia hofu zaidi ni kuona hata yale matokeo yaliyowekwa nusu bado hayaendani na matokeo yaliyopo kwenye mbao za matangazo. waliowengi kwa sasa wanawaza jinsi ya kusafiri kurudi chuo ili kuhakiki matokeo yao ili makosa yasije jirudia kwenye transcript zao na vyeti.
Aidha kumekuwepo na uzembe unaofanywa na idara ya ICT ambao haujurikani chanzo ni nini hasa kwa kuwekea mzaha mambo muhimu kama matokeo ya mtu hali inayoweza kupelekea kuharibu GPA ya mwanachuo husika.
Pia kwa wahitimu wa mwaka wa tatu wa chuo hicho kitengo cha elimu wamekubwa na sitofahamu baada ya kupata taarifa kuwa wanahitajika kwa mtaaluma tarehe 22/08/2014 chuoni hapo. walio wengi wanawaza nauli ya kusafiri hadi Moshi na kurudi zaidi ikiwa ni kuwaza sehemu za kulala na kula kwa kipindi hiki ambacho wengi enzi za nyuma walitegemea mkopo (boom) na kwa sasa hawana.
Hakika elimu ya chuo hicho mwisho wake umekuwa mchungu japo wahenga walisema mchumia juani hulia kivulini ila hili jua limekuwa kali sana.
Ushauri chuo kingeangalia watu wa kuajiri kulingana na taaluma ya kufanya kitu maana hiyo ni taasisi kubwa na inategemewa na watu. Mfano wa kero nyingine ni pale ambapo wengi walilipia pesa za transcript za semester tano lakini chs ajabu mpaka sasa hawajapatiwa sababu eti hazijaandaliwa.