Mazungumzo ya Sudan Kusini yakwama
Jaribio la hivi karibuni la kutaka kurejesha hali ya amani huko Sudan Kusini limevunjika saa ishirini na nne tu baada ya kuanza kwa mazungumzo.
Wasuluhishi kutoka jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo ya mashariki na nchi za pembe ya Africa IGAD wameeleza kuwa waasi wameshindwa kushiriki katika mazungumzo hayo katika siku ya pili ya kutafuta suluhu mkutano unaofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa.
Wasuluhishi hao wameomba uungwaji mkono kutoka mataifa mbalimbali ili kutia msukumo mazungumzo hayo na hivyo kuwashawishi waasi kurejea katika meza ya mazungumzo.
Hata hivyo pamoja na jitihada za kutafuta amani ya Sudan Kusini bado mapigano yameendelea , na zaidi ya watu milioni moja na nusu hawajulikani walipo kutokana na mapigano hayo yaliyoibuka mwishoni mwa mwaka wa jana, baada ya Rais Salva Kiir kumshutumu aliyekua makamu wake Riek Machar,kwa kuchochea mapigano hayo.