Agnatio Jeremia aliyekuwa mfanyakazi kitengo cha ulinzi katika lindo la Ngara GF kilichokuwa kikisimamiwa na kampuni ya ulinzi ya Victoria Support Service Ltd ya Mwanza aliachishwa kazi gafla baada ya kampuni hiyo kupunguza maenoe ya malindo hivyo kupelekea mwajiri kuvunja mkataba na wafanyakazi wake.
Aidha katika barua ya kuachishwa kazi iliyosainiwa na meneja wa kampuni hiyo Ndugu Mbonesho George inaonesha kwamba mfanyakazi huyo anapaswa kulipwa pesa zake zote za mishahara ya miezi mine (4) aliyokuwa akidai, malipo ya miezi mitatu ya likizo, pia mafao yake aliyokuwa akichangia PPF na kiinua mgongo chake kwa mujibu wa mkataba aliosaini. Jumla ya deni lote ni shilingi 1249000/= pesa ya kitanzania.
Aidha anaiomba serikali kuingilia kati dhidi ya hizi kampuni binafsi zinazotesa watu kwa kutowapatia haki zao za msingi kama kudhurumiwa mishahara yao ya kazi na mafao yanayokatwa na kupelekwa PPF ambacho ni chombo cha ulinzi wa jamii (social security scheme) lakini badala yake kinatumiwa kudhurumu haki za wateja wao.
Mwisho ndugu, Agnatio Jeremia ana hati zote za madai hayo ikiwa ni barua ya kuachishwa kazi, mkataba wa kazi na zaidi yeye na wenzake wanajipanga kwenda mahakamani kuishtaki kampuni hiyo maana wapo walinzi au wafanyakazi wenzake zaidi ya mia mbili waliofanyiwa unyama huo na hiyo kampuni ya Victoria Support Service Ltd ya jijini Mwanza.
CHANZO: AGNATIO MIBURO JEREMIA.