MICHEZO:-REAL MADRID YAINASA SAINI YA KIPA SHUJAA WA COSTA RICA KEYLOR NAVAS
MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda mlango na shujaa wa Costa Rica katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka
huu nchini Brazil, Keylor Navas.
Navas amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika ushindani na kipa Iker Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine Diego Lopez anasepa zake.
Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni inasomeka: "Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita ijayo""Mchezaji atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania) kwenye uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya".