Mtu katikati: Samir Nasri anatazamiwa kutangaza kustaafu soka la kimataifa.
SAMIR Nasri hajaweza kuweka wazi kabisa dalili za kustaafu soka la kimataifa
kufuatia kuenguliwa katika kikosi cha kocha Didier Deschamps kilichoshiriki kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
Nasir aliachwa kwenye kikosi hicho kwasababu Deschamp alidai kuwa nyota huyo hachezi kwa kujitolea katika timu ya taifa kama anavyofanya akiwa na klabu yake ya Manchester City.
Demu wa Nasir, Mhispania Anara Atanes alijibu mapigo kwenye mtandao wa Twita na kuitukana Ufaransa na kocha wake akisema: ‘F*** france and f*** deschamps! What a s*** manager!’ (hutujaona haja ya kutafsiri maneno haya kwasababu ya maadili).
Suala hili lilimkatisha sana Nasir ambaye aliondoka tena kikosini katika fainali za mwaka 2010 nchini Afrika kusini na alifungiwa mechi tatu baada ya kumtukana mwandishi wa habari katika fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2012.

Nasri amefurahia mapumziko ya majira ya kiangazi baada ya kuzikosa fainali za kombe la dunia









 
Top