Msanii wa muziki wa kizazi kipya Recho amesema kuwa pamoja na umaarufu wake anahitaji sana kurudi shule ili aweze kuongeza uwezo wake wa kuimba...

Recho alisema kuwa anaamini baada ya kutimiza ndoto yake ya kurudi shule mambo yake mengi yatakuwa mazuri kwani hata muziki wake utazidi kufika kimataifa ikiwa ni pamja na kuimba nyimbo ambazo zinaweza kuinua uchumi wa taifa.....

"Shule lazima nirudi kwani kule ndo kwenye mipango na maisha mazuri, naelewa bila shule mabo mengi tunakuwa tunafanya lakini tunakosea, mashabiki wangu ambao wanatamani kuniona nikirudi shule wanaamini kuwa ntafanya hivyo kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kazi yangu," alisema Recho.
 
Top