Ngombe mwenye kilo 1000 kutoka Mafinga Iringa akipita mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mashindano ya mifugo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Nzuguni wa Nanenane mjini Dodoma August 6, 2014.
Ngombe wakiwa wamejipanga katika maonyesho ya mifugo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Nanenane wa Nzuguni uliopo Dodoma August 6, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mapishi ya pilau la kuku ya Mama Irene mamuya (kulia) wa Chako ni Chako Dodoma katika maonyesho ya wakulima Nanenane yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nzuguni Dodoma August 6, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani kukagua banda la Wizarahiyo katika monyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Nzuguni Dodoma August 6, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).