Waziri wa Ujenzi John Magufuli amesema Serikali inatarajia kuongeza kivuko kingine cha kuvusha watu Kigamboni ambacho kitagharimu shilingi bilioni 3.7 wakati ujenzi wa daraja ukiendelea.

Anasema daraja linalojengwa sasa hivi litakamilika June 2015 badala ya July kama ilivyokua imefahamika mwanzoni ambapo tayari Mkandarasi ameshalipwa shilingi Bilioni 117 kati ya 214 za kukamilisha mradi wote limeandika gazeti la Tanzania Daima.
Nalo gazeti la HabariLEO August 9 2014 limeandika >> Magufuli abana wenye magari Kigamboni, ataka wasisumbue abiria wa Pantoni asubuhi na jioni, wenye haraka watakiwa kuzunguka Kongowe – Mbagala, ni agizo la muda mfupi baada ya kivuko kilichopo kuzidiwa.
 
Top