Wajumbe wa Bunge la katiba watakiwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.
Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Mh Jaji mstafau Joseph Warioba amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba waendelee kushirikiana ili kufanikisha watanzania kupata katiba mpya na watambue kuwa dira yao kubwa ni taifa na siyo vyama vyao vya siasa.
Mh Warioba ameyasema hayo katika mdahalo uliondaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere na kuwahusisha waliokuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba ulikuwa na mada ya umuhimu wa kuzingatia mambo ya msingi katika mchakato wa katiba mpya.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere amesema japo yeye ni mwanachama wa CCM lakini chama chake kupitia serikali iliyopo madarakani kimekosea mambo kadhaa ikiweo kuficha baadhi ya vitabu vilivyotolewa na tume hiyo na hivyo kuwanyima fursa baadhia ya watu kufuatilia mchakato huo.