Dotto Ndanga mwenye miaka 31 mkazi wa eneo la Mkwawa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa amefariki baada ya kugongana na dereva mwenzake akiwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajili T:349 CCW aina ya SKYMARK RACER.
Aidha amesema marehemu amefariki wakati akitokea chuo kikuu cha Mkwawa kuelekea maeneo ya Iringa mjini ambapo alikuwa akijaribu kuipita pikipiki nyingine iliyokuwa mbele yake iliyokuwa ikiendeshwa na Joyce Kiwale ambaye amekimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo chanzo kikiwa ni mwendo kasi wa marehemu.
Hata hivyo kamanda Mungi amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta dereva aliyekimbia baada ya kutokea tukio hilo kwa uchunguzi zaidi pia anatoa wito kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatioa sheria za usalama barabarani ili kupunguiza ajali zinazoweza kuepukiaka.