Mtu mmoja amejeruhiwa kwa kupigwa risasi katika shamba la Durubay katika kijiji cha Mkwaya Kata ya Mingoyo Mkoani Lindi. Mtu huyo ametambulika kwa jina la Laulent Antony ambaye inasadikiwa alikwenda kuokota korosho katika shamba la mwanakijiji ajulikanae kwa jina la Saida, walinzi wawili pia wa eneo hilo wameweza kujeruhiwa kwa mapanga katika miili yao na wananchi wa eneo hlo baada ya kumjeruhi kwa risasi ya moto kijana huyo. Wananchi wa kijiji hcho wamefunga barabara kwa kutumia magogo ya miti ya mikorosho.
ENDELEA KUWA NASI KWA TAARIFA KAMILI.
Na Ahmeid Abdul Aziz wa Lindi yetu.com