Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewashushia kipigo baadhi ya wafuasi wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema na kutumia mabomu kuwatawanya wanachama waliokuwa wakijiandaa kufanya maandamano katika ofisi ya Chadema mtaa wa Ngoto mjini Morogoro.
Askari wajeshi la polisi walionekana kwa wingi kuzunguka ofisi za Chadema za mjini Morogoro ambapo wafuasi wa Chadema walikua katika maandalizi ya kufanya maandamano huku wakionekana na mabango ya kupinga kuendelea kwa vikao vya bunge la katiba ambapo kabla ya mandamano hayo baadhi ya vijana walipigwa na kisha kupakizwa katika gari la jeshi la polsi ambapo baadhi ya viongzi wa Chadema wamelalamikia jeshi la polisi kutumia nguvu huku wengine wakilalamikia baadhi vifaa vya ofisi kupote wakati wa vurugu hizo.

Katika hatua nyingine baadhi ya askari wa jeshi la polisi walitaka kuingia kwa nguvu katika ofisi za Chadema kuwachukua baadhi ya watuhumiwa walio kuwa wakifanya vurugu ambapo walizuiwa na viongozi wa Chadema na mambo yalikua hivi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul akizungumzia tukio hilo amekiri jeshi la polisi limetumia mabomu kuwatawanya wafuasi wa Chadema na wamelazimika kufanya hivyo kwa kua walikua wakiandamana bila kufuata utaratibu kwa kukika maagizo yaliotolewa na jeshi la polIsi nchini na katika tukio hilo watu watano wanashikiliwa na wamefikishwa mahakamani.

CREDIT: ITV








 
Top