LIGI KUU VODACOM, VPL, Msimu wa 2014/15 inaanza rasmi Jumamosi Septemba 20 kwa Mechi 6 na Jumapili ipo Mechi moja.
Jumamosi, Mabingwa Watetezi, Azam FC, watakuwa Nyumbani Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kucheza na Polisi Morogoro ambayo imerejea tena VPL Msimu huu baada ya kuporomoka Daraja.
Yanga, ambao Msimu uliopita walikamata Nafasi ya Pili, watakuwa Ugenini huko Morogoro kucheza na Timu ngumu Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Hiyo Jumamosi, Mechi nyingine zitarindima kwenye Miji ya Shinyanga, Tanga, Mlandizi na Mbeya.
Jumapili, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam itakuwepo Mechi ya ‘Wapwa’ wakati Simba itakapocheza na Coastal Union.
VPL itafunga rasmi Msimu wa 2014/15 hapo Tarehe 18 Aprili 2015.
LIGI KUU VODACOM
RATIBA-Mechi za Ufunguzi
Septemba 20
Azam FC v Polisi Moro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Yanga [Jamhuri, Morogoro]
Stand United v Ndanda FC [Kambarage, Shinyanga]
Mgambo JKT v Kagera Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandizi]
Mbeya City v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]
Septemba 21
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
MECHI ZA MOTO
DABI ya Kariakoo:
12-10-14 Yanga v Simba [Uwanja wa Taifa, Dar]
08-02-15 Simba v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar]
DABI ya Mbeya:
03-01-15 Mbeya City v Prisons [Sokoine, Mbeya]
11-04-15 Prisons v Mbeya City [Sokoine, Mbeya]
Mechi nyingine za Mvuto:
21-09-14 Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar]
09-11-14 Yanga v Azam FC [Uwanja wa Taifa, Dar]
20-12-14 Coastal Union v Yanga [Mkwakwani, Tanga]
01-01-15 Azam FC v Simba [Uwanja wa Taifa, Dar]
17-01-15 Coastal Union v Simba [Mkwakwani, Tanga]
TBA Azam FC v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar]
28-03-15 Yanga v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar]
12-04- Simba v Azam FC [Uwanja wa Taifa, Dar]