Sherehe hiyo imefanyika jana siku ya alhamisi ya tarehe 25/09/2014 ambapo wito umetolewa kwa wazazi kuhakikisha wanawaendeleza watoto wao watakaofaulu kujiunga na elimu ya sekondari. Aidha akiongelea suala la kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokaidi kuwasomesha watoto waliofaulu sekondari, Afisa mtendaji wa kijiji cha Murukukumbo ndugu Jonifasi Gideon alisema kuwa utaratibu huo upo na mfano mzuri ni wazazi waliokaidi kuwasomesha watoto waliohitimu miaka ya nyuma. Akiongea mwalimu mkuu wa shule hiyo  Majaliwa Stephano alisema kuwa hata kwa watakaoshindwa kuendelea na sekondari kuna fursa ya kujiunga na elimu ya ufundi na sayansi kimu inayotolewa shule hapo.
 Wahitimu wakiingia jukwaani.


Wahitimu wakicheza show


 
Top