MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NKUSUBILA KAMINYONGE (70) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI AINA YA SMG MAENEO YA MKONO WAKE WA KUSHOTO CHINI YA BEGA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO MAENEO YA SOWETO, MTAA WA KATI, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIVUNJA GETI LA NYUMBA NA KISHA KUINGIA NDANI NA KUVUNJA MLANGO WA CHUMBA ALICHOKUWA AMELALA MAREHEMU NA KISHA KUMPIGA RISASI.
WAKATI WATU HAO WANAVAMIA NYUMBA HIYO, MAREHEMU ALIKUWA AMELALA NA MUME WAKE AITWAYE OSIA MALAMBUGI (72) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO AMBAYE ALISHTUKA BAADA YA KUSIKIA MLIO MKUBWA WA RISASI NA KUKUTA MKE WAKE AMEPIGWA RISASI NA WATU HAO AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.

HAKUNA KITU CHOCHOTE KILICHOCHUKULIWA/KUPORWA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO KUFAHAMIKA, UPELELEZI UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MSAKO UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU HAO WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO

 
Top