Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rasimu iliyotengenezwa na bunge maalumu la katiba imekiuka haki ya kimsingi ya maoni ya wananchi kwa kuondoa vipengele muhimu vya Rasmu iliyowasilishwa katika bunge.
Jaji Warioba amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika sherehe za miaka 19 za kituo cha LHRC ambapo amesema maoni mengi yaliyowekwa ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya viongozi na sio yanayoleta maridhiano kwa Wananchi.

Hata hivyo Warioba amesema kuwa baada ya mabadiliko yaliyofanyika wananchi ndio wenye uamuzi kuhusu hatma ya rasimu ya katiba iliyoundwa na Bunge Maalumu la katiba.
 
Top