Picha ya mtoto Tedi Station aliyepotea
Mtoto anayefahamika kwa jina la Tedi au Foresi Station (11) mkazi wa Kabanga wilayani Ngara na mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kabanga alipotea siku ya jumatatu ya tarehe 22/09/2014 majira ya saa kumi jioni baada ya kutoka shuleni. Waliondoka na mtoto mwingine anayeitwa Kibinda Jackson Senkamiye (10) naye mkazi wa Kabanga. Wazazi wao walitoa taarifa kituo cha polisi cha Kabanga ambapo waliwashauri kutoa tanagazo baada ya siku saba na kwa sasa siku saba zimetimia tangu kupotea kwa watoto hao. Watoto wote wawili ni wa kike na bado ni wanafunzi, aidha huyo Tedi ni mweusi kiasi, mwembamba, mrefu kidogo, anaongea lugha ya kiswahili na Kihangaza. Aliyewaona au atakayewaona sehemu yoyote hasahasa maeneo ya Ngara, Kahama na Mwanza awasiliane na mzazi wa mtoto kupitia namba 0787402704 au 0685164861. Pia unaweza kuwasiliana na blogger kwa namba 0766378713 au utoe taarifa kituo chochote cha Polisi kilicho Karibu nawe ili wawasiliane na kituo cha polisi cha Kabanga.
Ukisoma tangazo hili mfahamishe na mwenzako.