Bao za Mbrazil, Andey Coutimho, Dakika ya 34, na Simon Msuva, Dakika ya 68, zimewapa Yanga SC ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Prisons kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa Leo Septemba 28,2014,Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa Bao 1 na Prison kumaliza wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Jacob Mwakalobo kupewa Kadi za Njano mbili na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu.

Licha ya upungufu huo, Kipindi cha Pili Prisons walisawazisha Bao katika Dakika ya 65 lakini Dakika 3 baadae Simon Msuva akafunga Bao la ushindi.

Nako huko Chamazi, Uwanja wa Azam Complex, Kagera Sugar imewachapa Wenyeji wao Bao 2-0 katika Mechi nyingine ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa hii Leo Septemba 28,2014.

Bao za Kagera Sugar zilifungwa na Salum Kanoni kwa Penati na Rashid Mandawa.


Mshambuliaji wa Yanga, Genilson Santana 'Jaja' akimpongeza mwenzake Andrew Coutinho (wa kwanza kushoto) aliyeifungia Yanga bao la kwanza dhidi ya Prisons katika Uwanja wa Taifa, Dar leo Septemba 28,2014.


Kikosi cha Prisons kilichoanza dhidi ya Yanga leo Septemba 28,2014.

MATOKEO LIGI KUU TANZANIA 2014/2015.

Septemba 27,2014.

Simba SC 1 - 1 Polisi Moro 

Azam FC 2 - 0 Ruvu Shooting 

Mbeya City 1 - 0 Coastal Union 

Mgambo JKT 0 - 1 Stand United 

Mtibwa Sugar 3 - 1 Ndanda FC

Septemba 20,2014.

Azam FC 3 - 1 Polisi Moro 

Mtibwa Sugar 2 - 0 Yanga SC

Stand United 1 - 4 Ndanda FC

Mgambo JKT 1 - 0 Kagera Sugar 

Ruvu Shooting 0 - 2 Tanzania Prisons 

Mbeya City 0 - 0 JKT Ruvu 

Septemba 21,2014.

Simba 2 - 2 Coastal Union


Kikosi cha Yanga kilichoiua Prisons ya Mbeya mabao 2-1.
MSIMAMO VPL 2014/2015.

MSIMAMO VPL 2014/2015.

NATIMUPWDLFAGDPTS
1Azam FC22005146
2Mtibwa Sugar22005146
3Mbeya City21101014
4Ndanda FC21015433
5Tanzania Prisons21013213
6Kagera Sugar21012113
7Mgambo JKT21011103
8Stand United210124-23
9Yanga210123-13
10Simba20203302
11Coastal Union201123-11
12JKT Ruvu201102-21
13Polisi Moro201124-21
14Ruvu Shooting200204-40
 
 
Top