Hawa ni mashabiki wa soka wakiwa kwenye foleni kubwa kuingia kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro,tayari kuwaona wenyeji Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga SC kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2014/2015 iliyoanza rasmi leo Septemba 20,2014.
Ligi kuu soka VODACOM Tanzania bara Msimu wa 2014/15 imeanza rasmi hii Leo Septemba 20,2014 na Mabingwa Watetezi Azam FC kuanza kwa ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya Polisi ya Morogoro huko Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati Yanga SC wakisulubiwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Jamhuri, Morogoro.

Bao za Azam FC zilifungwa na Didier Kavumbagu, Bao 2, na Aggrey Moses na Bao pekee la Polisi lilifungwa na Bakari.

Huko Morogoro, Bao za Mtibwa Sugar zilipigwa na Mussa Mgosi, Dakika ya 15, na Ame Ali, Dakika ya 82.

Kikosi cha Mtibwa Sugar .



Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar .


Nao Ndanda FC imeonyesha imepania kufanya kweli, baada ya kuichapa Stand United kwa mabao 4-1.

Ikiwa ndiyo mechi ya kwanza kwa timu hizo ya Ligi Kuu Bara, Stand ikiwa nyumbani Kambarage imelala kwa mabao hayo 4-1.


Wageni Ndanda walipata mabao yao kupitia Paul Ngalema, Nassor Kapama na Ernest Mwalupani.


Wakati wenyeji ambao walijitahidi kurekebisha mambo walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Salum Kamana.

Mechi ilikuwa nzuri nay a kuvutia lakini wageni ndiyo walioonyesha soka la kuvutia zaidi.

Maafande wa JKT Ruvu wameonyesha kweli walipania kuanza ligi kwa kishindo baada ya kuishika nyumbani timu ya Mbeya City.

Katika mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine, kila timu upande ulionyesha soka la kuvutia, lakini mwisho hakuna aliyeona nyavu za mwenzake.

Kipindi cha kwanza kilikuwa na mashambulizi ya zamu lakini kipindi cha pili, Mbeya City wakabadilika na kuanza kushambulia sana.

Wachezaji wake, Deus Kaseke, Mwagane Yeya na Themi Felix walionekana kupania kushinda lakini mambo yalikuwa magumu.

Kiungo Jabir Aziz alionyesha kuwapa wakati mgumu Mbeya City akishirikiana na washambuliaji Realiants Lusajo na Iddi Mbaga.

Hadi mwisho, Mbeya City ambao walishika nafasi ya kwanza msimu uliopita, walikuwa hawajapata kitu na wageni wao hali kadhalika.

Ruvu Shooting imeanza ligi vizuri kwa kuwatungua maafande wa Magereza, Prisons kwa mabao 2-0.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mabatini Mlandini, Pwani, wenyeji ndiyo walikuwa sawa zaidi.

Vijana wa David Mwamwaja walijitahidi kusawazisha mabao hayo katika kipindi cha pili, lakini wapi.

Jumapili, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam itakuwepo Mechi ya ‘Wapwa’ wakati Simba itakapocheza na Coastal Union.


LIGI KUU VODACOM RATIBA


Septemba 21,2014.


Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]


Septemba 27,2014.


Simba v Polisi Moro [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]


Mtibwa Sugar v Ndanda FC [Manungu, Morogoro]


Azam FC v Ruvu Shooting [Azam Complex, Dar es Salaam]


Mbeya City v Coastal Union [Sokoine, Mbeya]


Mgambo JKT v Stand United [Mkwakwani, Tanga]


Septemba 28,2014.


JKT Ruvu v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]


Yanga v Prisons [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
 
Top