Yaya Toure
Kiungo wa kati wa timu ya manchester City katika ligi ya soka ya Uiungereza Yaya Toure amesema kuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo ni sharti waonyeshe umahiri wao wakati watakapochuana na Chelsea baadaye siku ya jumapili.
Mancity ambao walishindwa kwa bao moja kwa sufuri dhidi Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika mechi za kuwania taji la kilabu bora barani ulaya wamewachwa kwa pointi sita na Chelsea ambao kwa sasa wanaongoza ligi hiyo.Wachezaji wa Liverpool
Wakati huohuo timu ya liverpool ilipoteza mechi yake ya tatu kati ya tano ilizocheza katika ligi ya Uingereza msimu huu baada ya West Ham kuicharaza mabao matatu kwa moja katika uwanja wa nyumbani wa Upton Park.
Mabao ya mapema ya West Ham yaliofungwa na Winston Reid na Diafra Sakho yaliichanganya Liverpool ambayo ilipata bao la kufuta machozi kupitia Raheem Sterling.
Katika matokea ya mechi nyingine arsenal iliirindima Aston Villa mabao matatu kwa bila ugenini.
Southanmpton nayo ikaifunga Swansea bao moja lililoingizwa kimywani na mchezaji wa timu ya taifa ya kenya Victor Mugubi Wanyama huku QPR ikitoka sare ya mabo mawili kwa mawili dhdi ya Stoke City.