Maelfu ya wanafunzi mjini Hong Kong wameanza maandamano ya juma moja kupinga mpango wa serikali ya Uchina ya kuwakagua wagombea wa uchaguzi wa kiongozi wa eneo hilo.
Wengi walikongamana katika chuo kikuu cha Uchina kilichopo mjini humo.
Waliishtumu Uchina kwa kukiuka makubaliano ya kidemokrasia wakati Uingereza ilipoikabidhi uchina eneo hilo mnamo mwaka 1997.
Walimu 300 wa chuo hicho pia wanaunga mkono maandamano hayo,ambayo yanalenga kuanzisha kampeni kubwa ya uasi wa raia.
Uchina imekubali kufanya uchaguzi wa moja kwa moja mnamo mwaka 2017,lakini ina uwezo wa kuwachagua wagombea wachache wanaounga mkono Uchina.
Mkutano mkubwa zaidi umepangwa kufanyika mwezi ujao na kundi la Occupy Central ambalo limeahidi limeahidi kufanya maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa HOng kwa niya ya kufunga eneo lote la katikati ya jiji hilo.