Mabingwa wa kombe la CCM 2014/2015-wilaya ya Kasulu,mkoani Kigoma,Timu ya Kasulu United ambayo iko hapa wilayani Ngara mkoani Kagera katika ziara yake ya kimichezo ya siku mbili toka Jana Septemba 20,2014, ilipocheza na Rulenge White Stars mjini Rulenge na kuwafunga bao 2-0,Leo Septemba 21,2014 ikishuka mara ya pili uwanja wa Kokoto mjini Ngara ,imeambulia kipigo cha bao 3-1 kutoka Ngara Stars.

Mabao ya Ngara Stars yalifungwa kitalamu na kuvutia Watazamaji kupitia kwa Edward Kijanjali bao 2 na Abdul Karim.

Ngara Stars jana Septemba 21,2014 ,walikuwa wanacheza mchezo huo wa Kirafiki wa Ujirani Mwema na Bingwa wa Kombe la Chama cha Mapinduzi CCM 2013/2014,Timu ya Kasulu United baada ya Jana Septemba 20,2014 kucheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa kirafiki na Timu ya mkoa wa Chankuzo nchini Burundi na kuwafunga bao 3-0.KUJUA ZAIDI MCHEZO HUO INGIA HAPA


Kikosi cha Ngara Stars jana katika Picha ya pamoja ndani ya Uwanja wa Kokoto mjini Ngara.

Kikosi cha Kasulu United leo katika Picha ya pamoja ndani ya Uwanja wa Kokoto mjini Ngara.

Utata nao wa Maamuzi ya Refa wa mechi ya leo Septemba 21,2014-Seif Upupu na Wasaidizi wake uliwatatiza wachezaji wa pande zote mbili wakati wa mchezo huo kama picha inavyoonyesha.


Kushoto ni Afisa Utamaduni na Michezo wilaya ya Ngara Salumu Bakari na wa tatu ni Katanga katibu mkuu chama cha soka wilaya -NDFA wakifatilia mchezo huo uwanja wa Kokoto mjini Ngara.

Katikati ni John Shimilimana,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,Kulia ni Alex Gashaza Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Ngara -NDFA wakifatilia mchezo huo uwanja wa Kokoto mjini Ngara leo Septemba 21,2014 na Ngara Stars kushinda bao 3-1 dhidi ya Kasulu United.

Kushoto ni Niniani Bakari Diwani viti Maalum CCM-Kata ya Kanazi na Mwanaharakati wa Soka la Wanawake wilaya ya Ngara akiwa sambamba na Waratibu wa Ziara ya Timu ya Kasulu United,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kasulu,Mberwa Abdalla na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kasulu,Masudi Kitowe wakishuhudia timu ya Kasulu United ikifungwa na Ngara Stars uwanja wa Kokoto.






 
Top