Mwanachama wa zamani wa Chadema, Bi.Batuli Abdallah akijieleza mbele ya wanahabari (hawako pichani)leo Septemba 30,2014.
Yassin Bahama aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chadema akizungumza.
Mohamed Ngulangwa aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) akivaa fulana ya chama hicho.
Mwenyekiti wa ACT, Hamis Chambuso akiwa ameshika kadi za Chadema zilizorudishwa na wanachama hao wapya.
Wajumbe na wanahabari wakiwa mkutanoni.
Chama cha siasa hapa nchini Tanzania cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT, leo Septemba 30,2014,kimewapokea wanachama wapya ambao wamehama toka vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Waliopokelewa ni Yassin Bahama aliyekuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa matofalini, Ujiji Kigoma, Batuli Abdallah aliyekuwa Katibu Mwenezi Bavicha katika Jimbo la Kawe, Ofisa na mwasisi wa chama cha Chauwa, Sylvester Kasonga pamoja na Engineer Mohammed Ngulangwa toka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza mbele ya GPL, eneo la Msasani Club, jijini Dar, Mwenyekiti wa Mkoa wa ACT, Hamis Chambuso amewakaribisha na kuwapongeza wanachama hao wapya kwa hatua waliyoichukua.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)