Hatimaye mahakama ya wilaya ya bunda mkoani mara imewachia kwa dhamana viongozi na wanachama kumi wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema baada ya kusota mahabusu kwa siku sita kufuatia kesi ilifunguliwa na jeshi la Polisi kwa kudaiwa kufanya mkusanyiko kinyuime cha sheria na kuhatarisha amani.
Wakizungumza muda mfupi baada ya viongozi hao sita wakiwemo wanachama wanne wa Chadema na CCM kupata dhamana hiyo kwa kusimamiwa na mawakili kutoka kampuni ya mawakili ya Ap ya jijini Mwanza, viongozi baadhi ya Chadema mkoa wa Mara na wilaya ya Bunda, wamedai kusikitishwa na nguvu kubwa zinatumiwa na vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani.
Hata hivyo mmoja ya mawakili hao kutoka katika kampuni ya uakili ya Ap ya jijini Mwanza Bw Afred Goyayi ameishukuru mahakama hiyo ya wilaya ya Bunda kutenda haki kwa kukubali maombi ya dhamani kwa watuhumiwa hao baada ya upande ya mashitaka kuweka pingamizi kuhusu dhamana hiyo.
Septemba 23 mwaka huu jeshi la Polisi liliwakamata viongozi na wanachama hao wa Chadema na CCM kwa madai ya kufanya maandamano ambayo yalizuiwa na jeshi la Polisi kisha kufunguliwa mashitaka ya kufanya mkusanyiko bila kibali kinyume cha sheria na kuhatarisha amani, kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo oktoba saba mwaka huu.