Lori aina ya Scania namba T 607 CWV Semi Taller (kama linavyoonekana katika picha) lililokuwa limebeba kokoto limeanguka katikati ya Barabara leo October 12,2014, katika eneo la Chalinze Mzee Mkoani Pwani na kuharibika vibaya.
Kwa mujibu wa Mashuhuda, ajali hiyo ametokea baada ya gari hilo lililokuwa likielekea Dar es Salaam, kuteleza kutokana na mvua iliyonyesha asubuhi ya leo mkoani humo.
Hata hivyo askari wa usalama barabarani walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuliondoa gari hilo ambalo limesababisha foleni kubwa ya magari yaliyokuwa yakitokea jijini Dar es Salaam kwenda mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na kuziba barabara.