Jukwaani ni Washabiki wa Taifa stars wakiisapoti vilivyo timu yao....Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepata ushindi mnono dhidi ya Benin wa mabao 4-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa Kalenda ya FIFA leo October 12,2014,jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo ,Taifa Stars hadi Mapumziko tayari ilikuwa inaongoza mabao 2-0,kwa mabao ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16 na kiungo Amri Kiemba dakika ya 39.


Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars,Juma Luizio akiipachikia bao la nne kwa timu yake katika mtangange wa kikataifa wa kirafiki dhidi ya Benin, katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu aliifungia Taifa Stars bao la tatu dakika ya 49 akimalizia krosi fupi ya Mrisho Ngassa aliyemtoka vizuri beki wa Benin.

Mshambuliaji wa ZESCO United ya Zambia, Juma Luizio aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Ngassa, aliifungia Stars bao la nne akimalizia kazi nzuri ya Ulimwengu aliyemtoka beki wa Benin.

Benin ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Suanon Fadel dakika ya 90.


Wachezaji wa Taifa Stars,wakishangilia ushindi wao huku wakiwaacha wapinzani wao wa Benin wakiwa hoi tena wakiwa hawaamini wanachokiona uwanjani hapo.



 
Top