Baadhi ya askari wa jeshi la mgambo wa kabanga wakijiandaa kuutoa mwili wa marehemu nje ya jengo la choo.
Dereva huyo aliyefahamika kwa jina la Rajab mkazi wa barabara ya 4 mjini Bujumbura nchini Burundi amekutwa amefariki dunia katika choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Kabanga Garden Hotel.
Dereva huyo alikuwa safarini jana tarehe 18/10/2014 akitokea Dar Es salaam kuchukua gari hiyo bandarini kuelekea Bujumbura nchini Burundi. Aidha inasemekana kwamba baada ya kufika eneo hilo la Kabanga garden hotel alipaki gari yake vizuri na kisha kuomba kwanza kwenda haja kujisadia kabla hajaandikisha chumba.
Umati wa  watu ukimiminika kushuhudia tukio hilo
Mwili wake umegundulika leo tarehe 19/10/2014 asubuhi na mtu aliyekuwa anaingia chooni humo kujisaidia. Jeshi la polisi la kituo cha Kabanga limefika eneo la tukio na kuthibitisha tukio hilo. Aidha vipimo vya daktari vimeonesha kuwa marehemu alikuwa mgonjwa hivyo ugonjwa huo ambao haukutajwa mara moja ndio umepelekea umauti huo ulomfika.
Gari mpya ya IT alokuwa nayo marehemu

 
Top