Kikosi cha Kabanga fc

Mchezo huo wa robo fainali ya kwanza ulichezwa jana tarehe 17/10/2014 katika uwanja wa kokoto mjini Ngara ukizikutanisha timu za Ngara stars na Kabanga fc.
Mchezo huo ulimalizika dakika 90 bila kupata mshindi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na hivyo waamuzi kuamuru kuongeza dakika 30 ili kuufanya mchezo kuchezwa dakika 120. Ngara stars walifanikiwa kupata gori dakika ya 117 na hivyo kujihakikishia kuendelea hatua ya nusu fainali kwa ushindi huo wa gori moja kwa bila dhidi ya kabanga fc.

Mashabiki wakisubiri kipindi cha pili kianze
Robo fainali nyingine itaaendelea leo tarehe 18/10/2014 ikizikutanisha timu za Benaco fc waliokuwa washindi wa kwanza kwenye kundi B na walimu fc waliokuwa washindi wa pili kundi A. Na hapo kesho trehe 19/10/2014 itachezwa robo fainali ya mwissho itakayozikutanisha timu za Ngara boys ambao ni washindi wa pili kundi B na Rulenge white stars ambao ni washindi wa kwanza kundi C.

Aidha baada ya robo fainali itachaguliwa timu ya best looser ambayo itaungana na timu tatu zilizoingia nusu fainali kucheza hatua hiyo ya nusu fainali.
 
Top