Polisi Mkoani Kagera imewafukuza kazi Askari wake watatu kwa kuweka picha za mahaba kwenye mitandao ya kijamii, wakiwa kwenye sare za jeshi hilo huku mwanamume akiwa amempakata wa kike wakipigana busu.
Askari hao walikuwa wanafanya kazi kikosi cha usalama barabarani Wilayani Missenye mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Henry Mwaibambe amesema picha hiyo sio ya kuchakachua na ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kwa kuwa kitendo hicho kimelidhalilisha jeshi la Polisi.

Askari hao na mwenzao aliyewapiga picha wametambuliwa na tayari wamefukuzwa kazi kwa kitendo hicho cha kulidhalilisha Jeshi la Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana October 09,2014,mjini Bukoba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Herny Mwaibambe alitaja askari walio kwenye picha hiyo ni Namba F.7788 PC Mpaji Mwamsumbi na WP 8898 PC Veronica Mdeme, wote wa Wilaya ya Missenyi.

Aliyewapiga picha ni askari mwenye namba G.2122 PC Fadhili Linga.

Kwa mujibu wa Kamanda, walipiga picha mwaka 2012 wakiwa kazini kabla ya kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali hivi karibuni ikionesha Veronica akiwa amemkalia Mpaji mapajani. 

Kamanda alisema picha hiyo inakwenda kinyume na maadili mema ya jeshi hilo.
 
Top