Kikosi cha Kabanga fc
Michezo mitatu ya ufunguzi wa ligi ya wilaya ya Ngara imechezwa leo tarehe 08/10/2014 katika viwanja vitatu ambavyo ni Kokoto mjini Ngara, Rulenge na Benaco. Katika uwanja wa Benaco, timu ya Benaco fc imeshinda kwa gori 2 kwa 1 dhidi ya timu ya Ngara boys ya mjini Ngara gori la ushindi la timu ya Benaco limepatikana kwa mkwaju wa penati baada ya ngome ya Ngara boys kufanya dhambi eneo la hatari.

Katika uwanja wa Rulenge, timu ya Ngara stars wametoshana nguvu kwa kufungana sare ya gori 1 kwa 1 na timu ya Rulenge white stars. Katika mchezo huo Rulenge white stars ndio wamekuwa wa kwanza kupata gori na hatimaye Ngara stars wamejipanga vizuri na kusawazisha gori hilo hadi kipenga cha mwisho matekeo yalisomeka Ngara stars 1 Rulenge 1.

Aidha mchezo mwingine uliochezwa uwanja wa kokoto mjini Ngara umeikutanisha timu ya Kabanga fc na walimu fc ya mjini Ngara, Mchezo huo umemalizika kwa sare ya gori 1 kwa 1. Gori la Kabanga fc limefungwa dakika ya 7 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji namba 9 Ezra Essau na gori la walimu fc limepatikana dakika ya 28 ya kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wao Ilakoze aliyepiga shuti kali lililomshinda gorikipa wa Kabanga Fc. Aidha mchezo huo umeharibiwa na mwaamuzi (refarii) Geofrey ambapo baadhi ya wapenzi wa mpira wilayani Ngara wamesema kitendo cha kutumia waamuzi ambao kidogo umri umeenda na wana muda mrefu hawajihusishi na michezo ndo kunapelekea kutokuelewana uwanjani. Pia baadhi ya wadau wa soka wanalalamikia kitendo cha timu za Ngara mjini kubebwa na waamuzi hasa zinapocheza na timu kutoka nje ya mji wa Ngara, wakikwepa kuhusisha uongozi wa chama cha mpira wilayani Ngara kuwa na walimu ndani yake, mchezo wa Kabanga fc dhidi ya walimu fc umeonesha dhahiri timu ya walimu kubebwa na mwaamuzi hadi kupata gori la kusawazisha. Mpira ni fair play ila kwa maamuzi ya marefa wetu wilayani Ngara tunaua sifa ya mpira ambapo badala ya kujenga urafiki na undugu tunachenga chuki miongoni mwa wachezaji.

Kikosi cha Kabanga fc
 
Top