Basi la Kampuni ya NBS lililokuwa linatoka Jijini Mwanza kwenda Mpanda, likiwa limeharibika vibaya baada ya kugonga punda jana October 09,2014, asubuhi na kupinduka katika eneo la Nzega Ndogo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kwamba mtu mmoja ambaye ni kondakta wa basi hilo amefariki dunia na majeruhi 12 walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega kwa matibabu Zaidi.
Picha juu na chini ni Basi la Kampuni ya NBS l likiwa eneo la tukio na limeharibika vibaya baada ya kugonga punda jana October 09,2014.
Punda aliyesababisha ajali hiyo jana October 09,2014, akiwa amekufa baada ya kugongwa na basi la NBS