.........Polisi wakibeba mwili huo.........
Katika hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso
Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana maramoja imeandikwa nini.
Tukio hilo limetokea Oktoba 13,2014, eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo.
Katika uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea usiku wa siku hiyo,kwani kutwa nzima ya siku hiyo hapakuonekana mtu ambae amekufa katika eneo hilo.
Mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi moja jirani na eneo la tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo anaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.
Habari Na:-Dj Sek.