Kijana mmoja mkazi wa Kimandolu jijini Arusha, (jina kapuni) mwenye umri wa miaka 18 amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru baada ya kubakwa na kisha kukatwa ulimi na mwanamke mmoja aliyekuwa akimtaka kimapenzi.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 6.30 usiku katika eneo la Tindigani, kimandolu, wakati mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la mama Abuu alipofika katika bar hiyo kama mteja na baadaye alimlazimisha mhudumu wa bar hiyo ambaye ni majeruhi kufanya mapenzi bila ridhaa yake.

Akiongea na mwandishi wa habari hii mfanyakazi katika bar hiyo, inayomilikiwa na mwenyekiti wa mtaa ,Joel Mbasha alisema mnamo majira ya usiku alikuja mwanamke huyo na kuagiza kinywaji huku yeye akimhudumia kabla hajamgeuzia kibao .

Alieleza kuwa ilipotimu majira ya saa 6.30 wateja waliisha katika bar hiyo na kuamua kufunga bar ,hata hivyo mwanamke huyo ndiye aliyebaki pekee akinywa pombe taratibu katika eneo hilo ndipo alipomlazimisha kufanya kitendo hicho ambapo alimziba mdomo kwa kutumia kinywa chake na baadae alifanikiwa kumng’ata ulimi na kuutema chini.

Majeruhi huyo kwa sasa hali yake bado mbaya kwani hawezi kuongea na muda mwingi anatokwa na damu nyingi hatua ambayo imewalazimu wahudumu katika hospitali hiyo kumwekea ndoo ya kutemea damu.

Jeshi la polisi mkoani Arusha limethibitisha tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
 
Top