Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, jana October 05,2014 ambapo yalipata mtafaruku baada ya Polisi kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.
Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu.

Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi usawa uko wapi, posho ya mjumbe wa Bunge la Katiba kwa siku shilingi laki tatu, mshahara wa mwalimu shilingi 370 kwa mwezi. No big results without big salary (Hakuna matokeo makubwa bila mshahara mkubwa)”.

Ujumbe huo ulikuwa ukifanya rejea ya viwango vya malipo ya Sh300,000 kwa siku ambazo walikuwa wakilipwa wajumbe wa Bunge Maalumu zikiwa ni Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao.

Hata hivyo bango hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu,Bw. Mizengo Pinda.
 
Top