Jeshi la Polis Mkoani Kigoma limemshikilia Abona Daniel (40) makazi wa kijiji cha Sigunga Tarafa ya Buhingu Wilayani Uvinza kwa kosa la kumjeruhi mke wake baada ya kumkata viwiko vya mikono kwa panga.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma,Japhari Muhamed amesema tukio hilo limetokea jana October05 baada ya Abona kumtuhumu mke wake ambaye ni Jasmini Kasimu (24) kuchukuwa pesa kiasi cha Tzs 400,000/= laki nne na kupeleka kwao bila makubaliano.

amesema kuwa,sambamba na kumpoiga mke wake,Abona akaamua kumkata viganya vya miko kwa kutumia panga na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo kamanda ameongeza kuwa hari ya majeruhi inaendelea vizuri na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani ili kujibu mashtaka yake,

Katika tukio lingine October03 Jeshi la Polisi mkoani kigoma limefanikiwa kumuuwa jambazi mmoja na kukamata bunduki aina ya SMG iliyokuwa na risasi 32 katika shambulizi la kurushiana risasi maeneo ya Kihinga katika kitongoji cha Msuka wilaya ya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Japhari Muhamed amesema tukio hilo limetokea Octoba03 ambapo Polisi wakiwa katika doria waliwakuta majambazi wanne wakisubiri magari ili kuyateka ndipo wakaanza kurushiana risasi,

amesema kuwa,baada ya kurushiana risasi kwa muda polisi walifanikiwa kumuua jambazi aliyekuwa na siraha anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka30.

Kamanda amesema kuwa,baada kumuuwa aliyekuwa na siraha wengine waliamua kukimbia kusikojulikana,na kuiacha bunduki hiyo ya SMG ikiwa na risasi32.
 
Top